Viongozi waandamizi wa UKAWA wamesema hawayatambui matokeo ya Urais yanayoendelea kutangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi NEC kwa madai kuwa yamehujumiwa
Kauli
hizo za kutoyatambua matokeo zimetolewa na Freeman
Mbowe,Profesa Safari na James Mbatia wakati wakiongea na vyombo
vya habari leo kuhusiana na mwenendo wa uchaguzi mkuu.
Mwenyekiti
wa Chadema, Mh Freeman Mbowe amesema serikali ya CCM imeamua
kuwatumia wakurugenzi,NEC na jeshi la polisi kupindua maamuzi
ya wananchi na kuamua kutangaza matokeo ya uongo.
Mbowe
ametumia muda mwingi kulilaumu jeshi la polisi kuwakamata Ma IT
wa Chadema waliokamatwa wakijumlisha matokeo ya Lowassa jijini
Dar es Saalam, huku professa Safari akieleza jinsi NEC
ilivyochakachua matokeo....
"Nimesikitishwa na taarifa za kukamatwa kwa vijana wenzetu Wataalamu Wenzangu wa IT waliokuwa katika vituo vya majumuisho ya kura za mgombea Urais UKAWA.
"Huu ni UONEVU dhahiri kabisa. Inauma zaidi kwa wao kunyimwa kabisa dhamana.Hii si HAKI.
"Sitaki kuamini tumefikia hapa,sitaki kuamini uonevu wa kiasi hiki unatendeka kwa manufaa ya kisiasa." Amesema Mbowe

Katika
tamko lake, Profesa Safari ametolea mfano jimbo la tandahimba
ambapo amesema, kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na NEC
katika jimbo hilo,Magufuli amepewa kura 49,098 huku Lowassa akiambulia 46,288
Kwa
mujibu wa Profesa Safari, matokeo halisi waliyoyakusanya toka
kwa mawakala wao yanaonyesha kuwa Magufuli ana kura 44,253 huku Lowassa akiwa na kura 44,537
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia amesema
NEC watachakachua matokeo lakini sio hisia za wananchi.
Post a Comment