Gari
la mmoja wa makampeni meneja wa mgombea ubunge Jimbo la Moshi Vijijini
kwa tiketi ya CCM, Dk. Cyrill Chami, limeshambuliwa na kuharibiwa vibaya
na wananchi wakilishuku kuwa na kura bandia.
Katika
tukio hilo lililotokea saa 10:00 alasiri katika kijiji cha Uru Kitandu,
meneja kampeni huyo wa Dk. Chami aitwaye Kizitto George, aliokolewa na
Polisi lakini wakati huo akiwa ameumizwa vibaya kwa kipigo hicho.
Gari
hilo aina ya Toyota Verosa namba T756 CPB liliharibiwa vibaya kwa
kuvunjwa vunjwa vioo, kung’olewa magurudumu yake, kuibiwa redio ya gari
na vifaa mbalimbali kung’ofolewa.
Katibu
wa zamani wa Mbunge Chami, Martin Mallya alilithibitishia gazeti hili
kutokea kwa tukio hilo akisema gari hilo halikuwa limebeba kura yoyote
ila kinachoonekana walikuwa wakimwinda muda mrefu. “Hivi ninavyoongea na
wewe niko hapa Polisi majengo ili kufuatilia nijue amepelekwa hospitali
gani ila nimeambiwa gari limeharibiwa vibaya,” alisema Mallya ambaye
aliwahi kuwa Diwani wa kata ya Okaoni Kibosho kwa tiketi ya CCM.
CREDIT: Mwananchi
Post a Comment