Pichani
juu na chini ni muonekano wa Jengo la kituo cha afya Kivunge Wilaya ya
Kaskazini "A" visiwani Unguja kilichojengwa na Mashirika ya Umoja wa
Mataifa.
Na Mwandishi wetu
BAADHI
ya Wananchi wa Kijiji cha Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” wameelezea
kuridhishwa kwao na huduma za afya zinazotolewa katika kituo kipya cha
afya cha Kivunge.
Kituo
hicho kimejengwa chini ya mradi wa Umoja wa Mataifa(UN) wa kuviwezesha
vituo vya afya mbali mbali nchi ambapo kituo hicho kinatoa huduma mbali
mbali za akina mama na watoto pamoja na masuala ya kutibu vidonda na
majeraha mbali mbali.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mkazi wa kijiji hicho, Kassim Haji Simai alisema
kituo hicho kimekuwa mkombozi wa wananchi kwani pindi panapotokea
mgonjwa wa ghafla ufika katika kituo hicho na kupewa matibabu ya haraka.
Alizitaja
changamoto kubwa iliyopo kituoni hapo kuwa ni pamoja na upungufu wa
madakta na wauguzi jambo ambalo baadhi ya wananchi ukaa muda mrefu
wakisubiri huduma kwani wagonjwa wanakuwa wengi kuliko watoa huduma.
“Tunawashukru
sana wafadhili waliojenga kituo hiki na serikali kwa ujumla kwani
wametusaidia sana huduma hizi tulikuwa tunazifuata mbali sana”, alisema
Haji.
Kwa
upande wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
alifika katika kituo hicho na kutembelea maeneo mbali mbali ya kituo
hicho na kuona ni jinsi gani kinatoa huduma kwa wananchi.
Alisema
kuwa ufanisi wa mradi huo unaongeza ushawishi kwa Umoja wa Mataifa
kuongeza zaidi msaada hasa vifaa vya kisasa vya huduma za afya pamoja na
wataalamu wa afya ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma za
afya kwa ufanisi zaidi.
“
Kituo hiki kinatoa huduma kwa wananchi wengi hivyo nitapeleka salamu
makao makuu ili tujadiliane na kuona ni jinsi gani tunaendelea kusaidia
kituo hiki hasa katika suala la vifaa vya kisasa na madaktari.”,
alifafanua Bw.Rodriguez.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitazama jengo la kituo cha
afya Kivunge alipofanya ziara fupi ya kukagua miradi mbalimbali
inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa visiwani Unguja ikiwa ni sehemu ya
sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuaznishwa. Kulia ni
Daktari wa kujitolea wa kituo cha afya Kivunge, Alexander Vogt.
Naye
Mratibu wa Mradi wa Health Improvement Project (HIP), Jabir James
alisema kituo hicho kinatoa huduma bora na zenye kukidhi mahitaji kwa
wananchi ambapo kwa siku wanapokea zaidi ya wagonjwa 100 hadi 200 hali
ambayo kitathimini ni kubwa kutokana na uwezo wa kituo hicho kimatibabu.
Alisema
kuwa bado wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa kuongeza vifaa na madaktari
ili kuhakikisha wanaongeza ufanisi katika utoaji wa huduma bora ili
kufikia dhana ya umoja wa mataifa katika masuala ya afya ya kuhakikisha
kila mwananchi anakuwa na uhakika wa kupata huduma bora za afya na
endelevu.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikagua maeneo mbalimbali ya
kituo hicho huku akiwa ameambatana na Mkuu wa ofisi ndogo ya Umoja wa
Mataifa Zanzibar, Anna Senga (nyuma ya Alvaro) pamoja na Mtaalamu wa
Mawasiliano na Mahusiano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu.
Post a Comment