KUNENEPEANA!
Na ‘kuumuka’ kwa muigizaji wa muda mrefu, Blandina Chagula ‘Johari’
kumezua gumzo na mishangao kwa wadau wengi wa filamu na burudani huku
wakihoji kwa undani mabadiliko hayo ya ghafla kwani siku chache
zilizopita Johari alikuwa habari ya mjini kutokana na kudhoofika kwa
afya yake.
Wakizungumza
na Amani hivi karibuni, baadhi ya mashabiki na wasanii mbalimbali,
walionekana kushangazwa na muonekano mpya wa Johari na wengine kufika
mbali kwa kuhusisha na madawa maalum ya kunenepesha.
“Mmh,
jamani, mbona Johari kanenepeana sana? Si ndiyo kusema maisha
yamenyooka zaidi? Lazima kutakuwa na jambo maana siku chache tu alikuwa
amekondeana sana, si bure,” alisema mmoja wa wasanii wa filamu ambaye ni
moja rafiki wa Johari.
Hata
hivyo, ‘kibinubinu’ wetu alimtafuta Johari ili kusikia chochote kutoka
kwake juu ya mabadiliko ya mwili wake ambapo kwa haraka alifunguka:
“Duh!
Ina maana watu wanashindwa kufuata mambo yao wanabaki kuchunguza
mabadiliko ya mwili wangu? Kwa sasa sina stress (mawazo) yoyote
nimeridhika na maisha hivyo lazima mwili wangu ubadilike, si kingine
zaidi,” alisema Johari.
Chanzo: GPL
Post a Comment