TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Agizo
alilolitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli la kutaka fedha zilizochangwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya
kugharamia hafla ya wabunge zipelekwe Katika hospitali ya Taifa
Muhimbili kwa ajili ya kununulia vitanda na magodoro ya wagonjwa
wanaolala chini limetekelezwa.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema fedha hizo zimefanikisha
kupatikana vitanda 300 vya wagonjwa pamoja na magodoro yake, shuka 600,
Baiskeli za kubebea wagonjwa na vifaa vingine na kwamba hivyo vyote
tayari vimepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Balozi
Sefue ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vitanda vyote
vinafungwa kesho jumapili na kwamba atakwenda kuvikagua siku ya jumatatu
vikiwa tayari vinatumiwa na wagonjwa waliokua wanakosa vitanda vya
kulalia na kulazimika kulala chini.
Wadau
mbalimbali walichanga fedha kiasi cha shilingi milioni 225 kwa ajili ya
kugharamia hafla ya wabunge baada ya uzinduzi rasmi wa bunge la 11
lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
aliagiza fedha hizo zitumiwe kwa kiasi kidogo kisichozidi shilingi
milioni 15 na nyingine zipelekwe hospitali ya Muhimbili kutatua tatizo
la uhaba wa vitanda.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU,
Novemba 21, 2015.
Post a Comment