TIMU
ya Azam FC imeendelea kuongoza kwa ubora miongoni mwa timu za Tanzania,
kwa mujibu viwango vya ubora vilivyotolewa na mtandao wa footballdatabase.com Novemba 15, mwaka huu.
Azam
FC inayoongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
(VPL), inakamata nafasi ya 334 Afrika ikiwa imepanda nafasi 88 baada ya kujizolea jumla ya pointi 1249.
Klabu
nyingine ya Tanzania iliyoorodheshwa kwenye mtandao huo ni Simba,
ambayo inafuatia katika nafasi ya 338 ikipanda nafasi 86 ikiwa
imejisanyia pointi 1247.
Ni klabu hizo tu za Tanzania zilizochaguliwa na mtandao huo, ambao uhusisha timu 405 kutoka Afrika.
Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika
mwaka huu, TP Mazembe kutoka DRC yenye urafiki wa karibu na Azam FC,
ndio kinara kwa upande wa Afrika ikiwa imejizolea pointi 1653 ikifuatiwa
na wapinzani wao Vita Club, El Merreikh (Sudan) na Esperance de Tunis
na Kaizer Chiefs.
Post a Comment