Baada
ya kukamilisha kununua vifaa mbalimbali vya utayarishaji wa filamu
kwaajili ya kampuni yake mjini Dubai, Baby Madaha amedai kukutana na
changamoto bandarini.
Ameiambia Bongo5 kuwa hali hiyo imesababisha mzigo wake kukaa kwa muda mrefu bandarini hapo.
“Nimekutana
na changamoto kubwa sana bandarini,@ amesema. “Kutoa kontena lako
mchakato umekuwa mkubwa mpaka umeniharibia ratiba zangu, ni usumbufu tu
wa TRA, mara leo wakague kesho utasikia kingine,” amesema Baby Madaha.
“Nashukuru
Mungu kuna baadhi ya vitu ambavyo tayari vimeshaingia na natarajia
kuanza kazi soon baada ya kukamilisha process zote.”
Bongo5
Post a Comment