STAA wa
filamu na muziki, Flora Mvungi ‘H.Mama’ amecheza filamu moja na mtoto
wake aitwaye Tanzanite, akisema anafanya hivyo ili kuonesha kipaji
alichonacho.
Akipiga
stori na gazeti hili, Flora alisema baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu
akilea, sasa amerudi rasmi na kazi yake hiyo inaitwa Mtegoni, aliyosema
itasisimua wengi.
Katika
filamu hiyo, licha ya mwanaye pia amewashirikisha mastaa wengine kadhaa
akiwemo Wastara. “Baada ya kimya kirefu, sasa narejea na kazi hii
itakuwa mtaani muda si mrefu,” alisema.
Post a Comment