KATIBU
wa Bunge Dk.Thomas Kashilillah amesema kuwa, hadi sasa hajapokea barua
ya mbunge yeyote ya kukataa kupokea posho za vikao vya Bunge (Sitting
alowances).
Ni
siku motu imepita baada ya Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu
alidai kuiandikia barua ofisi ya bunge kueleza kuwa, hatochukua posho
hizo na badala yake zielekezwe katika maendeleo ya jimbo.
Dk.
Kashilila amesema, ofisi yake iko wazi, tayari kupokea barua ya mbunge
yoyote ambaye anakusudia kuandika barua ya aina hiyo kwa ajili ya
kufanyiwa kazi kulingana na maudhui hayo.
“Sisi
tupo ofisini na hatujapokea barua yoyote, hatuwezi kufanya kazi kwa
kutumia magazeti au mitandao ya kijamii kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa
tunakosea.
“Kama
kuna mtu anataka asipokee hiyo posho, tutaona jinsi ya kufanya lakini
hatuwezi kumzuia mtu asifanye vile anavyotaka, ni matakwa ya mtu mmoja
mmoja,” amesema Dk. Kashilila.
Amesema
iwapo mbunge ataandika basi itakuwa utashi wake mwenyewe na si wa
wengine “kwani wewe ofisini kwako ukisema hutaki kupokea mshahara,
watakulazimisha?, kwani wewe ukikataa mshahara na wengine watakataa”
alihoji.
Mbunge
mwingine ambayewahi kutangaza kutopokea posho hizo ni Zitto Kabwe
wakatia akiwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chadema.
Post a Comment