Watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameyateka
magari matano ya abiria na kuwapora mali mbalimbali zenye magari matano ya abiria na kuwapora mali mbalimbali zenye
thamani ya Sh1.3 milioni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 4
usiku eneo la Iguguno, wilayani Mkalama.
Alidai kuwa watu hao wakiwa wamebeba silaha za jadi, waliyateka magari hayo na kisha
kuwajeruhi madereva kabla ya kufanya uporaji huo.
Kamanda huyo aliwataja madereva
waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na Yasini Shemboko (40) mkazi wa Tanga, Ally Mchoba (40) na
Abood Juma (24) wote wakazi wa Dar es Salaam, Anold Adamu (23) mkazi wa Shinyanga na
Mathias Rameck (44) mkazi wa Mwanza.
Alisema majeruhi hao walipelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida walikopatiwa matibabu
na kuruhusiwa.
Kamanda Sedoyeka alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwafichua watu
wanaojihusisha na vitendo hivyo vya utekaji wa magari kwa kuwa wanaishi nao.
Alisema mpaka
sasa hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi wanaendelea na msako.
Post a Comment