Christian Bella na Ali Kiba
MUSA MATEJA
MKALI wa
dansi mwenye asili ya Kongo, Christian Bella amefunguka kuwa anajivunia
mafanikio makubwa waliyoyapata baada ya kufanikiwa kuingia studio na
mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba kuzalisha wimbo mkali ambao umeleta ladha
ya Dansi na Bongo Fleva, BongoDansi.
Mkali wa dansi mwenye asili ya Kongo, Christian Bella.
Akizungumza
na gazeti hili, meneja wa Bella aliyejitambulisha kwa jina la Simple,
alisema Bella na Kiba wamefanya ngoma hiyo kubwa kwenye Studio za Chedaz
Record zilizopo Mikocheni jijini Dar chini ya prodyuza Abidady ukiwa ni
utunzi wa Christian Bella.
Mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba
Alisema
wimbo huo ambao una ladha kali kutoka kwa wasanii hao wakali wa Dansi na
Bongo Fleva, tayari umeshakamilika na wameshaufanyia video ambayo
wameifanyia jijini Nairobi Kenya kwa Director Enock. “Lengo ni kuleta
kitu cha tofauti kwa mashabiki.
Wimbo
unakwenda kwa jina la Nagha-limia, tayari umeshaingia kwenye vituo
mbalimbali vya redio, utambulisho wa audio ataufanya Ali Kiba kwani
Bella yuko kwao Kongo kwenye matatizo ya kifamilia. Anatarajia kurejea
siku chache zijazo na akifika tu atafanya kazi ya kuachia video,”
alisema Simple.
Post a Comment