Dar es Salaam. Kanisa la Anglikana la Mtaa wa Kisanga B, Mivumoni Kinondoni, limekumbwa na operesheni ya bomoabomoa inayoendelea Dar es Salaam.
Bomoabomoa
hiyo iliyoanza juzi katika manispaa za Temeke na Kinondoni, inahusisha
ubomoaji wa nyumba zilizojengwa maeneo ya wazi na hifadhi za barabara
kinyume cha sheria.
Tangu kuanza
kwa operesheni hiyo katika Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, nyumba za makazi na
biashara 38, gereji tatu na sehemu ya kuoshea magari vilivyokuwa
vimejengwa kinyume cha sheria vimebomolewa.Hivi karibuni, Kamishna wa
wizara hiyo, Dk Moses Kusirika alitangaza kuanza kwa operesheni ya
kubomoa nyumba hizo na kuwa baada ya Kinondoni, watahamia wilaya
nyingine na mikoani.Katika Mtaa wa Kisanga B, Wazo – Mivumoni nyumba
tatu likiwamo kanisa hilo la Anglikana, zilibomolewa.Mwenyekiti wa Mtaa
wa Kisanga B, Mivumoni ambaye pia ni muumini wa kanisa hilo, Enock Kaisi
alisema hawakuwa na taarifa kuhusu operesheni hiyo na kwamba
walishangazwa kuona tukio hilo.“Nimeshangaa napigiwa simu saa 1.00
asubuhi kuwa kuna tingatinga na polisi wanabomoa nyumba tatu na kanisa
letu. Nilipofika eneo la tukio nikaambiwa tumelijenga kwenye eneo
lisiloruhusiwa kisheria, japo kulikuwa na kibali cha kuendesha kanisa,”
alisema.Mmoja wa wakazi wa mtaa huo aliyekumbwa na mkasa huo, Rehema
Sudi alilalamikia hatua hiyo akisema hakupewa taarifa.Hata hivyo,
alisema eneo lake halikustahili kuguswa kwa sababu ana vielelezo vyote
vinavyoonyesha yupo kihalali na hakuvamia eneo hilo kama Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inavyodai.Wamekuja saa moja asubuhi
bila kunipa taarifa nikawauliza kosa langu nini mbona nina uthibitisho
unaonyesha eneo hili siyo la wazi, wakanijibu nimevamia na ndani ya
dakika 10 nitoe vyombo vyangu.“Binafsi ninawashangaa kwa sababu
ninamiliki eneo hili kihalali tangu mwaka 2000... lakini nashangaa leo
(jana ) ninaambiwa niondoke,” alisema Sudi huku akiwaonyesha wanahabari
vielelezo alivyodai vinaonyesha kuwa ni mmiliki halali wa kiwanja
hicho.Aliiomba Serikali kumpatia eneo mbadala baada ya kumvunjia kwa
kuwa hana mahali pa kuishi na familia yake: “Nina familia sijui leo
(jana), tutalala wapi naomba Serikali iniangalie kwa jicho la
tatu.”Kutokana na mshtuko wa ubomoaji huo, wapangaji wawili mmoja akiwa
mjamzito ambao hawakujulikana majina yao walizimia na kupelekwa
hospitali.Akizungumzia kanisa, Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni
anayesimamia ubomoaji huo, Baraka Mkuya alisema: “Tumebomoa kanisa moja
ambalo halikuwa kubwa kwa sababu lilijengwa kwenye hifadhi ya mto katika
eneo la Kisanga B.”Alisema hawakuwa na sababu ya kutoa taarifa kuhusu
operesheni hiyo kwa maelezo kwamba wavamizi wa maeneo hayo hawakutoa
taarifa wakati wakifanya ujenzi huo kinyume cha sheria. Alisema katika
eneo la Mbezi Jogoo, manispaa hiyo ilibomoa nyumba moja na sehemu ya
kuoshea magari.Basihaya – BunjuKatika eneo la Basihaya – Bunju, baadhi
ya wakazi, walianza kubomoa nyumba zao baada ya kupata taarifa juu ya
kuwapo kwa operesheni hiyo ili kuokoa samani za ndani, bati, madirisha,
milango na mbao.Mwenyekiti wa mtaa huo, Malinusi Ndule alisema nyumba 15
zilibomolewa na wananchi wenyewe na kwamba, tingatinga lilipofika
liliambulia nyumba tatu.“Tulipata tetesi kuwa watakuja kwa hiyo wananchi
wakaanza kubomoa ili kupisha eneo la barabara walilokuwa wamevamia,”
alisema.Mhandisi Mkuya alisema wakazi wa eneo hilo walikuwa wamelipwa
fidia mwezi mmoja uliopita na kutakiwa wahame.Baadhi ya wamiliki wa
nyumba kwenye eneo hilo walisema kuwa walibambikiwa maeneo hayo na
wamiliki wa zamani, baada ya kubaini kuwa eneo hilo ni
barabara.Imeandikwa na Bakari Kiango, Tumaini Msowoya na Salma
Nganogera.
Post a Comment