Marehemu Maulidi Shaban enzi za uhai wake.
Suzan Kayogela na Chande
Abdallah INAUMA SANA! Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Maulidi
Shaban (21) ameuawa kwa kuchomwa kisu na rafiki yake aliyetambulika kwa
jina moja la Dotto (16) mkazi wa Kigogo jijini Dar, kisa kikiwa ni CD ya
filamu aliyomkodisha. Tukio hilo lilitokea Novemba 10 majira ya saa
tatu usiku eneo la Kintiku ambapo Maulidi alikuwa na kibanda cha kuuza
na kukodisha CD. Chanzo chetu kilielezwa kuwa kijana huyo aliuawa
kikatili baada ya kumshtakia Dotto kwa bibi yake kwa kutolipwa pesa wala
kurudishiwa CD yake.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo.
“Alipofika nyumbani kwao
alimkuta bibi yake Dotto na kumwambia kila kitu na alipoondoka majira ya
usiku ndipo Dotto na rafiki yake walimfuata Maulidi kibandani kwake na
kumtishia kisu. Alipotaka kukimbia ndipo rafiki yake Dotto anayetajwa
kwa jina la James alimpiga mtama na kuanguka hapo ndipo alipochomwa
kisu. “Watu walijitokeza kumpa msaada kwa kumpeleka kituo cha polisi
maana alikuwa amejeruhiwa kifuani na mkononi, hali yake ilikuwa mbaya
sana na alipokimbizwa Hospitali ya Amana, walipewa rufaa kuelekea
Hospitali ya Muhimbili lakini alifariki akiwa anapatiwa matibabu,”
kilisema chanzo hicho. Akizungumza na mwandishi wetu, Mjumbe wa Serikali
ya Mtaa wa Kigogo Kati, Ibrahim Said alisema tukio hilo limewafikia na
tayari kesi imefunguliwa katika Kituo cha Polisi Magomeni na upelelezi
unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwasaka watuhumiwa.
Mwili wa marehemu ulisafirishwa kuelekea mkoani Tanga kwa mazishi. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Post a Comment