Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari
mara baada ya Wabunge wa CCM kupitisha jisha la Spika.
Katibu wa NEC (CCM) Itikadi na Uenezi ambaye pia ni mbunge wa Mtama, Nape Nnauye alisema “Kamati ya Wabunge wote wa CCM imekamilisha kazi yake ya kwanza kuchambua na kupitisha moja kati ya majina matatu yaliyoteuliwa na Kamati Kuu.
Katibu Mkuu wa CCM akihutubia kwenye kikao maalum cha wabunge wa CCM kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
Aidha amesema katika kata 14 zilizofanya uchaguzi mdogo katika jimbo hilo CCM imepata kata 10 na upinzani kata 4.
Katibu Mkuu wa CCM akipokea pongezi alizopewa na wabunge wa CCM kwa kazi nzuri iliyowapa CCM ushindi mkubwa katika uchaguzi uliofanyika oktoba 2015. Sehemu ya wabunge wa CCM walioshiriki kwenye kikao maalum cha uchaguzi wa Spika kutoka Chama Cha Mapinduzi. Mbunge Mteule wa Nzega mjini Hussein Bashe akizungumza na Mbunge mteule wa jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye pamoja na Jerry Slaa (katikati) kabla ya zoezi la upigaji kura kwenye ukumbi wa NEC.
Katibu wa NEC (CCM) Itikadi na Uenezi ambaye pia ni mbunge wa Mtama, Nape Nnauye alisema “Kamati ya Wabunge wote wa CCM imekamilisha kazi yake ya kwanza kuchambua na kupitisha moja kati ya majina matatu yaliyoteuliwa na Kamati Kuu.
“Kama tulivyoona wagombea wawili walijitoa, hivyo Job Ndugai
amepitishwa kwa kauli moja kugombea nafasi ya uspika. Tunamuombea kura kwa
sababu sifa zote anazo, bila shaka hakutatokea mgombea wa upinzani atakayezidi
sifa zake,” alisema Nape.
Mbunge
wa Jimbo la Kongwa Ndugu Job Ndugai akiongea na waandishi wa habari nje
ya ukumbi wa NEC baada ya jina lake kupitishwa na wabunge wa CCM.
Katibu Mkuu wa CCM akihutubia kwenye kikao maalum cha wabunge wa CCM kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
KATIBU
mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) ndugu ABDULRAHMAN KINANA amefungua
kikao cha kamati ya wabunge wa CCM huku akiwahimiza wabunge hao kufanya
kazi ili kutekeleza kauli mbiu ya rais dr JOHN MAGUFULI ya hapa kazi
tu.
Akifungua kikao hicho leo mjini Dodoma ndugu KINANA amesema ili kuendana na kauli mbiu hiyo nilazima wabunge wote wafanye kazi.
Amesema
kazi waliyonayo kwa sasa ni kuwazungukia watanzania ambao wamewaamini
kwa kuwa njia pekee ya kutafsiri imani hiyo ni kuwatumikia kwa nguvu
zote.
Ndugu KINANA amewapongeza wabunge hao kwa
kutafuta kura nyingi za rais juhudi ambayo imekiletea chama heshima
kubwa na kuwahakikishia kuwa ofisi yake itaandaa siku maalum kabla ya
bunge linalofuata ili kuwapa majukumu ya namna ya kuwatumikia wananchi.
Amesema
kazi kubwa kwa wanasiasa ni kutekeleza ilani ya uchaguzi waliyonayo
kazi ambayo ana imani kuwa wabunge hao wataitekeleza ipasavyo.
Awali
akimkaribisha katibu mkuu,katibu wa wabunge wa CCM mama JENISTA
MUHAGAMA amesema kikao hicho nimaalum kwa ajili ya kuchagua jina moja la
atakayegombea nafasi ya uspika wa bunge la Jamhuri ya Tanzania kutoka
katika majina matatu yaliyopitishwa na kamati kuu ya halmashauri ya CCM
jana.
Majina hayo yaliyopitishwa ni la naibu
spika mstaafu JOB NDUGAI,mbunge wa Afrika Mashariki ABDULLAH ALLY MWINYI
na naibu mwanasheria mkuu wa serikali TULIA ACKSON MWASANSU ambaye
ameteuliwa na rais kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya Tanzania.
Uchaguzi
huo unasimamiwa na wajumbe wa kamati kuu ya CCM ambao ndugu WILLIAM
LUKUVI,MAUA DAFTARI na JERRY SILAA ambapo jina moja litakalopatikana
litapelekwa kesho bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura na wabunge wote.
SHUKRANI
CHAMA
Cha Mapinduzi(CCM) kimewashukuru watanzania kwa imani kubwa
waliyoionyesha katika uchaguzi mkuu uliopita uliowezesha kuwapa
ushindi wabunge wa chama hicho kwa asilimia 74.8.
Akifungua
kikao cha kamati cha wabunge wa CCM kilichofanyika ukumbi wa white
house mjini Dodoma katibu mkuu wa chama hicho ndugu ABDULRAHMAN KINANA
amesema kitendo hicho kimedhihirisha imani kubwa waliyonayo watanzania
kwa CCM.
Amesema watanzania wametafsiri imani
kwa kukipa kura CCM na kusema katika majimbo tisa yanayofanya uchaguzi
mdogo tayari CCM imeshinda katika jimbo la Lulindi lililopo mkoani
Tanga.
Katibu Mkuu wa CCM akipokea pongezi alizopewa na wabunge wa CCM kwa kazi nzuri iliyowapa CCM ushindi mkubwa katika uchaguzi uliofanyika oktoba 2015. Sehemu ya wabunge wa CCM walioshiriki kwenye kikao maalum cha uchaguzi wa Spika kutoka Chama Cha Mapinduzi. Mbunge Mteule wa Nzega mjini Hussein Bashe akizungumza na Mbunge mteule wa jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye pamoja na Jerry Slaa (katikati) kabla ya zoezi la upigaji kura kwenye ukumbi wa NEC.
Credit: CCM Blog
Post a Comment