Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Handeni Mjini wamempigia kura na kumchagua tena mgombea ambae alishinda awali Omari Abdallah Kigoda katika uchaguzi uliofanyika wilayani humo leo baada ya kamati kuu ya CCM Taifa kutaka urudiwe.
Akitangaza
matokeo hayo Mwenyekiti aliyesimamia uchaguzi huo Dk Maua Daftari
alisema kuwa wajumbe wote kwenye mkutano walikuwa 690 na waliopiga kura
ni 660 na uchaguzi ulikuwa wa wazi na haki na hakukuwa na tatizo lolote.
Alisema
Omari Kigoda amepata kura 402 na mgombea mwenzake Hamisi Mnondwa
alipata kura 257 huku kura moja ikiharibika na kufanya jumla ya kura
zote kuwa ni 660 hivyo kumtangaza Omari kuwa mshindi katika kura halali
259.
Awali
kabla ya uchaguzi huo mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho Taifa
Abdallah Bulembo alisema kuwa sababu kubwa ya kurudiwa uchaguzi huo ni
kutokana na mshindi wa kwanza na aliyemfuatia kushindwa kuvuka nusu ya
idadi ya wapiga kura hivyo hawakufika katika vigezo vinavyotakiwa.
Mgombea
huyo anatarajiwa kwenda kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwa msimamizi
mkuu wa uchaguzi jimbo la Handeni Mjini kesho na kuirudisha ambapo
tarehe tano wataanza kampeni rasmi.
Post a Comment