Na Chalila
Kibuda,Globu ya Jamii
MKUU wa
Wilaya ya Kinondoni,Paul Makonda amesema
wananchi ambao hawajaweza kupata haki zao katika mahakama za mwanzo wanaweza
kutumia kamati ya maadili.
Makonda
ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam,Makonda amesema kuwa watu wengine wanakosa haki katika mahakama na
hawajui wanaweza kupata haki sehemu gani kutokana na mwenendo wa kesi
ilivyoendeshwa.
Makonda
amesema kamati hiyo inawajibu wa kuangalia mwenendo wa maadili ya hakimu na
ikibanika kamati inaweza kuchukua hatua.
Amesema kuna
baadhi ya wananchi wanapewa hukumu za kesi lakini mwenendo wa kesi haujui na
mwisho wa siku anakosa haki kutokana na baadhi ya watu kutumia mahakama vibaya.
Makonda
amesema sheria ya Usimamizi wa Mahakama
Na.4 ya mwaka 2011 sehemu 51(1) kutakuwa na kamati ya mahakama ya
wilaya ambayo mwenyekiti wake ni Mkuu wa
Wilaya.
Aidha amesema wengine wanaounda kamati hiyo ni
Hakimu Mkazi wa Wilaya au msimamizi wa Wilaya ,Katibu wa Tawala wa Wilaya (DAS) ambaye anakuwa Katibu wa Kamati
hiyo,Kiongozi wa dini mmoja ambaye atateuliwa na Mkuu wa Wilaya ,mtu mashuhuri
wa wilaya ambaye ni mwadilifu.
Hata hivyo
amesema katika kamati hiyo maafisa wawili watateuliwa na Jaji anayesimamia .Kamati hiyo
itawajibika kupokea na kuchunguza malalamiko yaliyowasilishwa na wananchi
kuhusu mahakama na kuwasilisha ripoti kwa tume..
Post a Comment