Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CCTV YAMUUMBUA DIAMOND PLATNUMZ


Imelda Mtema na Musa Mateja
AIBU! Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amejikuta kwenye aibu nzito kutokana na kamera za CCTV alizofunga nyumbani kwake kuonesha ufuska anaoufanya na warembo tofauti wanaoingia na kutoka ndani ya mjengo huo, Risasi Mchanyiko linakumwagia ‘ubuyu’ kamili.


Chanzo makini kilicho ndani ya familia ya Diamond kililiambia gazeti hili kuwa kutokana na msanii huyo kubadilisha wanawake kila kukicha baada ya mzazi mwenzake Zari (Zarinah Hassan) kurudi Afrika Kusini hivi karibuni, alilazimika kumuita fundi kwa ajili ya kuzitengeneza kamera hizo kwa kuzifuta picha zote chafu.
“Yaani tangu Zari ameondoka nyumba ya Diamond imekuwa kama danguro kwani anabadili wanawake kila kukicha ambapo huwa wanaingia ndani ya mjengo wake ambako wanakunywa, wakishakolea kinywaji wanajikuta wakimalizana hukohuko jambo ambalo kamera alizofunga ndani zinarekodi kila tukio hali iliyosababisha amwite fundi.
Chanzo kinatiririka kwamba kutokana na Zari kuwa na utaalam wa kamera hizo, Diamond alilazimika kumwita fundi ili amsaidie kuzifuta picha zisizofaa zilizokuwepo ili hata kama ikitokea Zari amerudi kwa bahati mbaya, asizikute kwani itakuwa shida.
Chanzo chetu kinasema fundi aliyeitwa nyumbani hapo alijionea sinema ya bure kutokana na mambo mengi yaliyokuwemo ndani ya kamera hizo za ulinzi.
Ili kuleta mzani wa habari, paparazi wetu alimtafuta Diamond ambapo alipopatikana, alikana kuwepo kwa tukio hilo.
“Siyo kweli bwana. Wanaosema hivyo watakuwa wanataka kuniharibia tu kwa mtu wangu Zari,” alisema Diamond.

TUJIKUMBUSHE
Katika moja ya gazeti ndugu na hili, liliwahi kuripoti habari ambayo mama Diamond, Sanura Kasimu ‘Sandra’ na dada wa msanii huyo, Esma wakikiri kwamba ndani ya nyumba hiyo baada ya Zari kuondoka, wanamkaribisha mwanamke yeyote kuingia na akizingua, ataondoka kumpisha mwingine.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top