Katika hali isiyo kuwa ya kawaida Chama cha Demokrasia na Maendeleo mkoani Shinyanga leo kimedai kwamba Jeshi la Polisi mkoani humo limefanya maandamano ya Chadema bila kujijua.
Kwa
mujibu wa baadhi ya viongozi wa chama hicho walidai kupokea taarifa
kutoka kwa uongozi wa juu wa chama hicho ukiwataka kufanya maandamano
leo nchi nzima ya kupinga ushindi wa Dkt. John Pombe Magufuli kwa madai
kuwa demokrasia imebakwa katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu
uliofanyika tarehe 25 oktoba 2015.
Katibu
wa Chadema wilaya ya Shinyanga mjini George Kitalama amesema kwamba
chama hicho kimefanikiwa kufanya maandamano kupitia jeshi la polisi
lililozunguka mji mzima kuwasaka wanachama wa chadema na kuambulia
patupu.
“Tulipanga
kufanya maandamano leo Novemba 03,2015 mji mzima wa Shinyanga lakini
polisi ndiyo wamejitokeza kufanya maandamano wakiwa na magari yao kila
mtaa.”Alisema Kitalama.
Kufuatia
taarifa ya Chadema kutaka kufanya maandamano katika maeneo mbalimbali
nchini Askari wa Jeshi la Polisi wamekuwa katika misururu ya magari
yakiwemo ya maji ya kuwasha wakizunguka kuwasaka waandamanaji kutoka
chama hicho ambao hawakufanikiwa kufanya maandamano hayo.
Jijini
Dares salaam Askari Polisi wakiwa kwenye punda na wengine wa doria
wameonekana katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo nyeti na yenye ofisi
nyingi za Serikali ikiwemo Posta.
Post a Comment