Aliyekuwa
katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Wilbroad Slaa ametoa tathmini yake kwa
siku chache za Rais John Magufuli alizoanza kazi katika Serikali ya
Awamu ya Tano na maamuzi aliyoyafanya.
Dkt.
Slaa ambaye alikuwa mgombea urais kupitia Chadema mwaka 2010, ameeleza
kuwa maamuzi ya kufuta safari za nje kwa watendaji wa serikali yaliwahi
kuchukuliwa na Rais wa Serikali ya Awamu ya kwanza, Mwalimu Julius
Nyerere.
Alisema
kuwa hata wapinzani walikuwa wakilalamikia gharama zinazotumika kwenye
safari za nje na kwamba yeye pia aliwahi kupendekeza safari hizo kufutwa
na badala yake watendaji waende vijijini kuchagiza maendeleo.
“Tulilamikia
safari za JK nje ya nchi. Na mimi niliwahi kusema kuwa tufute safari za
njena kuanza kwenda zaidi vijijini. Tuone naye kama katufa tu… na
badala yake tufanye nini. Ni siku mbili (Jumamosi) ofisini huwezi
kufanya tathmini ya maana,” alisema.
“Tathmini
hii kwa kawaida hufanywa baada ya siku 100. Mwalimu alifanya hivyo.
Rais wa watu ni vyema akifanya hivyo. Ndiyo namna pekee ya kujua hali
halisi. Kwa Magufuli si ya kwanza, amefanya sana akiwa Waziri.”
Post a Comment