Katika
hali isiyotarajiwa na wengi, Katibu wa UVCCM wilaya ya Mbulu mkoani
Manyara, Bi. Anna Gideria ameteuliwa na Chadema kuwa mbunge wa viti
maalum.
Bi.
Gideria amejiuzulu nafasi ya ukatibu na kukabidhi barua yake kwa
mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Manyara, Bi. Regina Ndege baada ya
kutangazwa majina ya viti maalum na jina lake kuwa katika orodha ya
wabunge wa Chadema.
Akizungumzia
hatua hiyo, Bi. Ndege alieleza kuwa Bi. Gideria alipoteza imani na CCM
muda mfupi baada ya jina la waziri mkuu wa zamani, Frederick Sumaye
kukatwa katika kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea urais kwa tiketi ya
CCM.
Mwenyekiti
huyo alieleza kuwa Bi. Gideria alikuwa ‘Team Sumaye’ na aliomba likizo
ya mwezi mmoja baada ya jina la waziri mkuu huyo wa zamani kukatwa.
“Baada
ya Sumaye kutoswa, alipoteza imani na CCM na ilipofika wakati wa
kampeni mwezi Agosti aliandika barua ya kuomba likizo na kukabidhi
ofisini kwa mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya UVCCM wilaya ya Mbulu,” alisema Bi. Ndege.
Tukio
hilo limewashtua wananchi wengi wa Wilaya ya Mbulu ambao walikuwa
wanamuona Bi. Gideria kama kiongozi na mpambanaji wa CCM kuteuliwa kuwa
mbunge wa Chadema.
Zipo hisia za wananchi wengi kuwa huenda alikuwa anatumiwa kuihujumu CCM wakati wa kampeni.
Zipo hisia za wananchi wengi kuwa huenda alikuwa anatumiwa kuihujumu CCM wakati wa kampeni.
Post a Comment