Mwigizaji maarufu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Na Deogratius Mongela
YAMEMKUTA! Mwigizaji maarufu Bongo,
Kulwa Kikumba ‘Dude’ amelizwa kila kitu kwenye gari lake baada ya wezi
kuvunja kioo na kufanya uharibifu mkubwa kisha kutokomea na vitu hivyo.
Tukio hilo lililomchanganya Dude
lilijiri nyumbani kwake, Kiwalani jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo
jamaa hao waliruka fensi na kuvunja kioo cha nyuma kisha kutoa vitu
muhimu kwenye gari hilo aina ya Toyota Mark II.
“Ukweli sasa hivi nikisikia kelele za mwizi hata niwe naendesha gari, nitapaki na kwenda kutoa kichapo.
Wamenirudisha nyuma sana. Yaani
wamelisafisha kabisa gari langu kuanzia control box, redio, side mirror,
betri ya gari, taa zote, spea tairi, jeki na vitu vingine,” alisema
Dude akijiandaa kufungua jalada la kesi la kuwasaka wahusika.
GPL
Post a Comment