Katibu
wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa akizungumza na waandishi wa habari
kwenye ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba.
Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana leo, Novemba 02,2015 chini ya
Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete imejadili kwa kina
mapendekezo ya wana CCM walioomba ridhaa ya kugombea ubunge katika jimbo
la Handeni mjini.
Kamati
Kuu imetengua mapendekezo ya awali na kuagiza kurejewa kwa mchakato wa
kura za maoni kwa wana -CCM wawili walioongoza kura za maoni za awali.
Wana- CCM hao watakaopigiwa kura za maoni tena kesho Novemba 03,2015 ni pamoja na Omari Abdallah Kigoda na Hamis Hamad Mnondwa.
Aidha Kamati Kuu imeteua wajumbe watatu kusimamia zoezi hilo ambao ni Dk. Maua Daftari, Dk.Emmanuel Nchimbi na Alhaji Abdallah Bulembo.
Post a Comment