Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Bi. Zainabu Abdallah
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa
pongezi kwa Rais mteule wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa niaba ya
Shirikisho hilo leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Habari( MAELEZO).
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Bi. Zainabu Abdallah
(katikati)akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa
pongezi kwa Rais mteule wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa niaba ya
Shirikisho hilo leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Habari( MAELEZO). Kushoto
ni Katibu Msaidizi wa Shirikisho hilo Bw. Daniel Zenda na kulia ni Afisa Habari
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Frank Mvungi.Picha
na Frank Shija.
Frank Mvungi, MAELEZO
Rais
mteule wa Jamhuri Ya Muungano wa
Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa kwa kushinda kiti cha Rais
katika uchaguzi mkuu ulifanyika oktoba
2015 ikiwa ni kielelezo cha utendaji bora alionyesha katika kuwatumikia watanzania
kupitia nyazifa alizotumikia kabla ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa shirikisho la vyuo vikuu
Chama cha Mapinduzi (CCM) Bi Zainab Abdallah wakati wa mkutano na waandishi wa
Habari uliolenga kumpongeza Rais mteule
kwa tiketi ya chama hicho.
“Akifafanua
Bi Zainab amesema kuwa Rais Mteule Dkt. John
Pombe Magufuli ameshinda kiti cha Urais kwa kuwa ndiye mtu pekee ambaye
watanzania walikuwa wanamuhitaji ili aweze kuwaletea maendeleo kwa kuwa ni mchapa
kazi na ameonyesha kwa vitendo dhamira hiyo katika utumishi wake kwa miaka yote
iliyopita “alisisitiza Zainab
Bi.
Zainab amesema kuwa Rais mteule Dkt. Magufuli anayo dhamira ya dhati yakuwaletea
maendeleo watanzania ndiyo sababu hata kauli mbiu yake ililisisitiza kuwa “hapa kazi tu” hivyo ni wajibu wetu kama
watanzania kusisitiza umoja na mshikamano na kuondoa tofauti zetu ili tufanye
kazi kwa bidii ili kujenga uchumi wa taifa.
Akizungumzia
wasifu wa Rais Mteule Dkt. Magufuli; Bi Zainab
amesema kuwa ni mtu mwenye uzalendo,mwadilifu,mchapa kazi, na ambaye
watanzania wote wanamkubali kuwa anao uwezo wa kuliongoza Taifa katika kipindi
hiki.
Kwa
upande wa Uchaguzi mkuu Zainab amesema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki hali iliyowapa nafasi watanzania kuchagua
viongozi wanaowataka na kupelekea chama
cha mapinduzi kuongoza katika uchaguzi huo
kutokana na utendaji madhubuti wa viongozi wa Chama na Serikali.
Pia
Bi Zainab alitoa wito kwa watanzania kudumisha amani na umoja wa Kitaifa
ulioasisiwa na Viongozi wa kwanza wa Taifa hili ili kufikia maendeleo ya Kweli.
Shirikisho
la wanafunzi wa vyuo vikuu Chama cha
Mapinduzi (CCM) limekuwa likihamasisha
vijana kufanya kazi kwa bidii ili kujenga Taifa.
Post a Comment