Aliyekuwa
mbunge wa jimbo la Bukoba mjini balozi Khamis Kagasheki ametoa
tahadhari kwa baadhi ya watu wanotumia mitandao ya kijamii na kumtuhumu
kuwa baada ya kushindwa kupata nafasi ya ubunge ameondoa baadhi ya vitu
alivyovitekeleza akiwa mbunge wa jimbo hilo ikiwemo kudaiwa kuondoa
mtengo wa radi katika shule ya msingi kibeta, TV ya wananchi ya uhuru
platfom, gari la kubebea wagonjwa na kuzima umeme katika soko kuu la
kashai mjini Bukoba.
Balozi
Khamisi Kagasheki ametoa rai hiyo wakati akiongea na waandishi wa
habari mjini Bukoba ambapo amesema yeye hakuondoa kitu chochote
alichakitekeleza katika jimbo hilo bali hayo nimaneno yanayo enezwa na
baadhi ya watu waliopanga kumchafua na kueneza chuku dhidi yake, nahapa
anaeleza zaidi.
Balozi
Kagasheki amewataka watu wanaotumia nafasi hiyo kumchafua katika
mitandao ya kijamii kuacha mara moja kwani hatosita kuwachukulia sheria
za kimtandao wale wote wanao diliki kumchafua bila sababu yeyote.
Post a Comment