Aliyekuwa
M/kiti wa Chama cha wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba amedai kuwa
M/kiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar pamoja na Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar- ZEC wamekiuka katiba ya Zanzibar sura ya 9 hadi 11 pamoja na
Sheria ya Zanzibar ya kifungu cha 119 -hadi 129 kwa kufuta Uchaguzi
uliofanyika Octoba 25 mwaka huu ambapo ametoa wito wa kufanyika
mazungumzo ili kuepusha Zanzibar kutumbukia katika machafuko.
Akizungumza
na waandishi wa habari makao makuu ya CUF jijini Dar es Salaam kwa mara
ya kwanza tangu ajiuzulu unyekiti wa chama hicho,Prof.Lipumba amesema
dosari zinazodaiwa kutokea katika Uchaguzi huo zilipaswa zielekezwe kwa
ZEC na sio vyama vya siasa kwa kuwa vyama vyote vilifuata taratibu na
sheria na kanuni za Uchaguzi.
Amesema
kutokana na Uzoefu wake wa siasa za Zanzibar Tume ya Uchaguzi Zanzibar
pamoja na wadau mbalimbali wanaoitakia mema Zanzibar na Tanzania kwa
ujumla wanapaswa kuelekeza nguvu zao katika mazungumzo ya kuupatia
ufumbuzi mgogoro ulioibuka na sio kurudia Uchaguzi.
Aidha
Prof Lipumba kuachia kuibuka kwa mgogoro huo wa kikatiba na kisiasa
kunaweza kuirudisha Zanzibar nyuma pamoja na kumpa kazi rais mteule wa
Tanzania kuanza kushughulikia migogoro ya kisiasa badala ya maendeleo.
Wakati
huo huo Ujio wa Prof.Lipumba katika ofisi hizo kwa mara ya kwanza
umewakusanya mashabiki na vijana wa CUF katika ofisi hizo na kutoa
hisia zao.
Post a Comment