Chama
cha mapinduzi mkoani Mbeya kimekiri na kukubali kupoteza majimbo manne
ya uchaguzi na halmashauri mbili ambazo zimenyakuliwa na vyama vya
upinzani kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu, huku
kikimpongeza rais mteule wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa
kutangazwa mshindi wa ngazi ya urais kwenye uchaguzi huo.
Mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi ndiye ambaye ametoa
tamko hilo kwa niaba ya kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya CCM mkoa
wa Mbeya.
Baadhi
ya makada wa CCM wamesema kuwa ushindi wa Dk. Magufuli ni ushindi wa
watanzania wote kwa kuwa ni mtu mwadilifu na mwenye uwezo wa kuwaletea
wananchi maendeleo kutokana na tabia yake ya kupenda kuchapa kazi.
Baadhi
ya wananchi wamesema kuwa wanamtarajia rais Magufuri kuteua wasaidizi
wake walio makini ili aweze kukidhi matarajio ya wanananchi huku pia
wakitoa tahadhari kwa viongozi wazembe serikalini kuwa wajiandae kwa
mabadiliko na kuanza kujituma kufanya kazi baada ya kuapishwa kwa Dk.
Magufuli kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Post a Comment