Siku
moja kabla ya kuapishwa rais mteule wa serikali ya awamu ya tano Dkt
John Magufuli, aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha ukombozi
na maendeleo-CHAUMA- Bw.Hashimu Rungwe amepanga kufungua kesi mahakama
kuu ili iweze kutoa tafsiri ya inayotoa nguvu za kisheria kwa maamuzi ya
tume ya taifa ya uchaguzi kutohojiwa au kupelekwa mahakamani.
Akizungumza
na waandishi wa habari, aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha
ukombozi na maendeleo-CHAUMA- Bw.Hashimu Rungwe amesema katiba ya nchi
kifungu cha 107 kifungu kidogo cha kwanza kinasema mamlaka ya mwisho ya
utoaji haki itakuwa mahakama, huku ibara ya 74 kifungu kidogo cha 2
kinasema hakuna mahakama yeyote itakuwa na haki ya kisheria kuchungua
jambo lililo amriwa na tume ya uchaguzi hali inayotatanisha na kukiuka
demokrasia.
Katika
hatua nyingine waliokuwa wagombea ubunge katika jimbo la Kinondoni kwa
tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo, Bwana Karama Masoud na chama cha
mapinduzi Bwana Iddi Azzan pamoja na CHAUMA wamepanfa kufungua kesi za
kupinga matokeo ya uchaguzi kwa nyakati tofauti kwa madai ya kuwa
uchaguzi huo uligubikwa na ukiukwaji wa sheria ikiwemo kutishwa na
kuondolewa kwa baadhi ya mawakala katika vituo wakati wa zoezi la kupiga
kura pamoja na watu zaidi ya elfu 30 kunyimwa fursa ya kupia kura
katika vituo 19 vya kupigia kura.
Post a Comment