Wema
Isaac Sepetu ‘Madam’ ameangusha bethidei baab’kubwa ambayo imesheheni
kufuru ya aina yake na ‘kumtusi’ hadharani mpenzi wake wa zamani, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ kwa kumsema kuwa ni mtu wa kununua magari ya bei rahisi
hivyo hawezi kuifikia hadhi yake.
Sherehe
hiyo iliyosheheni mastaa kibao Bongo, ilifanyika katika ukumbi wa Wema
Sepetu uliopo ndani ya jengo la Millenium Towers, Kijitonyama jijini Dar
ambapo mwanadadahuyo alizua gumzo la aina yake baada ya kujizawadia
gari aina ya Range Rover lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200.
Ulipofika
wakati wa zawadi, mastaa na waalikwa mbalimbali walishindana kumtunza
mrembo huyo asiyechuja Bongo, vitu mbaimbali vya thamani, zikiwemo fedha
taslimu ambapo ‘wekundu wa Msimbazi’ walionekana kutapakaa katika eneo
maalum la kupokelea zawadi alilokaa Madam.
Alivyomtusi Diamond
Mara
baada ya kukamilika kwa zoezi la zawadi ndani ya ukumbi, ndipo Wema
alipowatoa nje waalikwa na kuwaonyesha gari lake jipya aina ya Range
Rover ambalo linasadikika kuwa litakuwa la kwanza kumilikiwa na msanii
wa kitanzania kutokana na thamani yake.
“This
is my new brand car, yaani ni mpya ya mwaka 2015, hakuna kenge yeyote
anayeweza kufuata nyendo zangu na yule ambaye alikuwa akijigamba eti
alinipa zawadi ya gari la elfu 30, nini na nini na hili aseme sasa maana
mimi si wa kuhongwa kila kitu,” alisema mrembo huyo, kauli
iliyoonyesha wazi kumlenga Diamond, ambaye aliwahi kumzawadia Wema gari
lenye thamani ya shilingi milioni 30 miaka michache iliyopita.
Post a Comment