MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro, kwa mara nyingine tena imeahirisha
hukumu ya kesi ya jinai inayomkabili Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za
Kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda.
Kesi
hiyo iliyotarajiwa kutolewa hukumu yake leo Jumatano na Hakimu Mkazi wa
Mahakama hiyo, Mary Moyo imeahirishwa na mshtakiwa amerudishwa rumande
baada ya hakimu husika kutokuwepo mahakamani hapo kwa madai kuwa
amekwenda kwenye kozi fupi ya kushughulikia kesi za uchaguzi mjini
Dodoma ambapo shauri hilo limelazimika kuahirishwa na Hakimu Mkazi,
Erick Rwehumbiza hadi Novemba 30, mwaka huu itakapofikishwa tena
mahakamani hapo.
Mshtakiwa
huyo anakabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo kutoa maneno yenye kuhimiza
imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa, mashtaka anayodaiwa
kuyatenda Agosti 2013.
Upande
wa mashtaka wa kesi hiyo unawakilishwa na Wakili wa Serikali
Mwandamizi, Benard Kongola, Sunday Hyera na George Mbalasa, wakati
upande wa Mshitakiwa unawakilishwa na Wakili Juma Nasoro, Abubakar Salim
na Bartholomeo Tarimo.
Awali hukumu ya Sheikh Ponda ilipangwa kutolewa tarehe 19 mwezi
10 kabla ya kuahirishwa tena na shauri hilo kupangwa kutolewa hukumu
Novemba 18 mwaka huu, kabla ya kuahirishwa tena hii leo hadi Novemba 30
Post a Comment