Vyama vinavyounda Ukawa wamesema wamemwandikia Spika wa Bunge, Job Ndugai barua kutaka kujua uhalali wa Rais John Magufuli kuhutubia Bunge bila matokeo Rais wa Zanzibar kujulikana.
Katika mkutano wao na waandishi leo, wamesema kuwa hawatakubali Katiba ivunjwe kwa kumruhusu Dk Shein kuingia bungeni wakati muda wake wa kushika madaraka ulishapita.
Katika hatua nyingine, Umoja huo umesema wabunge wa kambi ya upinzani bungeni wamekubaliana kuchanga kila mmoja Sh 300,000 kwa ajili ya kuchangia familia ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Geita, Alphonce Mawazo.
Uamuzi huo umetangazwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kwenye mkutano wa waandishi wa habari bungeni baada ya kikao cha wabunge wote wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Pia wamekubaliana Jumamosi ya Novemba 21, wataenda wabunge wote kuungana na viongozi wengine wa kitaifa kumzika marehemu Mawazo.
Post a Comment