371aa89c-105f-4856-b196-a664cc40943d
Baadhi ya “wagonjwa” walioambukizwa magonjwa ya dharura wakiwa nje ya Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali (EMD) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali (EMD) Imefanya mazoezi kwa ajili ya kupambana na majanga ya dharura mara yanapotokea katika maeneo mbalimbali hapa nchini. 
Mazoezi hayo yamefanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) chini ya Kitengo cha Magonjwa ya Dharura na Ajali na kuwahusisha madaktari, wauguzi wa hospitali hiyo na wataalamu kutoka hospitali nyingine. 
 Akizungumza katika zoezi hilo, Mkuu wa Idara hiyo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk Juma Athuman Mfinanga amesema lengo la zoezi hilo ni kuiandaa idara na hospitali hiyo ili kukabiliana na majanga pamoja na ajali mara zinapotokea hapa nchini. 
Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano kumekuwa kukitokea majanga makubwa pamoja na ajali ambazo uzoefu umeonyesha kwamba matukio hayo yanahitaji huduma bora na ambazo zinafanywa kwa wakati ili kuokoa maisha waliokumbwa na ajali hizo. 
Dk Mfinanga amesema kwamba zoezi hilo limefanikiwa vizuri kwa kuwa madaktari na wauguzi walitekeleza wajibu kwa wakati na ubora unaotakiwa kimataifa. 
Mazoezi mengine yamekuwa yakifanyika mara kwa mara kwa lengo la kuboresha huduma katika idara hiyo. Zoezi la leo si la kwanza bali mengine yamewahi kufanyika kwa ufanisi mkubwa.
4e086296-3d91-4d36-9ad4-ea3fc5c1c355Baadhi ya “wagonjwa”  walioambukizwa magonjwa ya dharura wakiwa nje ya Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali (EMD) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

82a23d09-5966-404f-924f-cc655bf10454
Wauguzi wakiwa wamembeba “mgonjwa” kwa ajili ya kupatiwa matibabu leo.
de10d3fa-3fbc-41cc-955d-3ce24d65db95  Dk Juma akizungumza na madaktari na wauguzi baada ya zoezi hilo kukamilika.
6733c51e-09a8-43bd-822e-4ebde9691fca Dk Juma akizungumza na madaktari na wauguzi baada ya zoezi hilo kukamilika

Credit: Mo Blog