JESHI
la Polisi mkoa wa Tanga linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za
kusafirisha kilo 462 za mirungi. Watuhumiwa hao ni dereva wa lori aina
ya Fuso lenye namba za usajili T 860 BYQ, mkazi wa Kibaha Picha ya Ndege
Alois na mkazi wa Mbauda mkoani Arusha, Rashid Juma (22).
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga, Zuberi Mwombeji akizungumza na waandishi wa
habari alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Novemba 11 mwaka
huu saa 11.45 alfajiri katika kijiji cha Kwamdulu, kata ya Kwamsisi
wilayani Korogwe.
“Gari
hilo lilikuwa likitokea mkoani Arusha kuelekea jijini Dar es Salaam
likiwa na magunia 23 ya mirungi sawa na kilo 462 ilikuwa imechanganywa
na maharage ili kuwazuga askari wasielewe kwamba ni mirungi lakini
kutokana na uwezo wa jeshi la Polisi tumeweza kuwabaini,” alisema.
Katika
tukio jingine, mkazi mmoja wa wilayani Mkinga, Shabani Aweso (35)
anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kusafirisha kilo 35 za mirungi.
Kamanda Mwombeji alisema Aweso alikamatwa Novemba 11 mwaka huu
akisafirisha mirungi hiyo kutoka mkoani Tanga kuelekea jijini Dodoma
ndani ya basi la Kampuni ya Tashrif katika kizuizi cha polisi kilichopo
eneo la Kabuku wilayani Handeni.
Alisema watuhumiwa wote wako mahabusu na uchung
Post a Comment