ALIYEKUWA mgombea
Mbunge katika Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo,
Kalama Masoud ‘Kalapina’ ameibuka na kupinga matokeo akidai atakwenda
mahakamani.
Akizungumza
na wanahabari leo Makao Makuu ya chama hicho Kijitonyama jijini Dar es
Salaam, Kalapina amesema matokeo yaliyompa ushindi mgombea wa chama cha
wananchi CUF ambaye alikuwa anaungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa
katiba ya wananchi UKAWA, Abdul Mtulia yalikuwa yamesheheni dosari
kubwa.
Amesema
katika kata 19 zilizopo katika Jimbo la Kinondoni, mawakala wake
walitishiwa na kulazimika kuacha kusimamia vituo walivyokuwa
wamepangiwa.Kalapina alitaja baadhi ya maeneo aliyodai mawakala wake
walitishiwa na baadae kuamua kuondoka kuwa ni kata za
kijitonyama,Tandale, Ndugumbi pamoja na Kigogo.
Alieleza
kuwa baada ya kubaini matatizo yote hayo alilazimika kugomea kusaini
karatasi ya wagombea ubunge, akiongeza kuwa hatua iliyobaki kwa sasa ni
kwenda kufungua kesi mahakamani.“Natarajia kwenda mahakamani kutaka
haki, kwa hiyo Jumatatu au Jumanne ijayo nakwenda kufungua kesi,”
alisema kalapina.
(NA DENIS MTIMA/GPL)
Post a Comment