Bashir |
JESHI la Polisi Jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Idara ya ya
Uhamiaji inaendelea kumchunguza mtu aliyekamatwa na hati za uraia wa
nchi mbili, anayedaiwa kuwa mwanaharakati wa siasa katika Chama cha
Demokrasia na Maendeleo. Anaandika Faki Sosi … (endelea).
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Bashiri Fenele Awale Ally, amekamatwa kutokana na utata wa uraia wake na jinsi ambavyo alivyokuwa akijihusisha na masuala ya siasa nchi Tanzania.
Kamanda Kova amesama kuwa mtuhumiwa huyo mwenye hati ya kuzaliwa ya
Tanzania yenye namba D063711 kwa jina la Bashiri Abdi Ally ambapo
ilionyesha kuwa amezaliwa Julai 11, 1969 katika hospitali ya Dodoma.
Lakini pia mtuhumiwa huyo amekamatwa na pasi ya kusafiria ya Kenya yenye
namba C000529 ambapo ilionyesha kuwa alizaliwa Nairobi Kenya Julai 11,
1969 kwa jina la Bashir Fenal Abdi Ally Awadhi.
“Kwa uchunguzi wa awali pamoja na kumbukumbu zenye utata mtuhumiwa
mtajwa sio raia wa Tanzania bali ni raia wa Kenya ambaye alipeleka
maombi idara ya uhamiaji lakini bado hajakubaliwa,” amesema Kamanda
Kova.
Wakati huohuo, Kamanda Kova amesema jeshi hilo limekamata waharifu saba
wakiwa bunduki aina ya SMG moja, bastola sita na bunduki aina ya Mark 4
Riffle moja na risasi 62.
Kamanda Kova amesema waharifu hao ambao wana viashiria vya ugaidi
walipanga kuvamia vituo vya polisi lakini kabla hawajatekeleza mipango
yao wamekamatwa.
Kova amesema kuwa mpaka sasa jumla ya majambazi wanahusishwa na ugaidi
wamefikia 74, wamekamatwa ikiwa pamoja na silaha 51 na risasi 890 za
silaha mbalimbali.
Picha ya mwanzo ni Huyo aliye mstari wa mbele alievaa nguo nyeusi aliyekunja mikono kifuani.
Picha ya pili ni hati yake ya ukaazi inayompa sifa ya mgeni aliyeruhusiwa kuishi nchini kwa kazi ya uwekezaji na wala sio kujihusisha na siasa.
Mgeni kujihusisha na masuala ya kisiasa ni kinyume cha Katiba na Sheria za nchi. Aidha amekiuka masharti ya kibali cha ukaazi alichopewa.
CHANZO : JAMII FORAM
Post a Comment