Na. Lilian Lundo - Maelezo
JESHI
la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam imefanikiwa kuwakamata
watuhumiwa 7 wakiwa na silaha 8 na risasi 62 kwenye msako uliofanyika
jijini Dar es salaam katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Akiongea
na waandishi wa habari leo, katika ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la
Polisi, Kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova
amesema wahalifu walidhani kuwa Jeshi la Polisi limeweka nguvu katika
uchaguzi mkuu na kusahau kufanya misako yake iliyokuwa ikifanya mara kwa
mara kama moja ya majukumu yake.
“Ukweli
ni kwamba Jeshi la Polisi lilijipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi mkuu
unafanyika kwa amani na misako mingine inaendelea kufanyika kama kawaida
kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na mikoa ya
jirani” Alisema kamanda Kova.
Kamanda
Kova aliongezea kwa kusema kuwa, Jeshi la Polisi kanda maalum
inashirikiana na mikoa ya jirani kuhakikisha kuwa watuhumiwa hao
hawapati fursa ya kukwepa mkondo wa sheria.
Aidha
alizitaja silaha zilizokamatwa kuwa ni SMG moja (1), Bastola sita (6)
na Mark 4 riffle moja (1) na risasi 62 ambapo mpaka sasa jumla ya
majambazi 74 wamekamatwa ikiwa ni pamoja na silaha 51 na risasi 890 za
silaha mbalimbali.
Kamanda
Kova amezidi kufafanua kuwa kutakuwa na msako mwingine mkali kuelekea
sikukuu za x-mass na mwaka mpya 2016, utakayofanyika katika mikoa ya
kipolisi ya Ilala, Kinondoni na Temeke wakisaidiwa na vikosi maalum
vilivyopo Kanda ya Dar es Salaam.
Msako
huo utajikita katika kuwakamata majambazi, magaidi, wanaojihusisha na
madawa ya kulevya, vibaka, wapiga debe, wanaouza pombe haramu, madanguru
yote ambayo pia huhifadhi wahalifu.
Post a Comment