KAMPUNI ya
SBC Tanzania Limited, watengenezaji na wasambazaji wa vinywaji baridi
imepunguza bei ya vinywaji vyake kutoka shillingi mia sita (600) hadi
mia tano (500) kwa chupa yenye ujazo wa Mililita 350 na 300.
Hayo
yamesemwa na Meneja Mafunzo na Uwezeshaji Bw.Rashid Chenja
(Pichani)alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam na kuongeza kuwa lengo la kupunguza bei ni kutokana na hali ngumu
ya uchumi iliyopo.
“Imekuwa
vigumu kwa mnywaji kuweza kudumu bei ya kinywaji akipendacho cha pepsi ,
gharama za maisha zinapanda kila mwaka na soda imekuwa ghali kiasi cha
wananchi wa kawaida kushindwa kumudu kununua soda hivyo kampuni imeamua
kupunguza bei” alifafanua Meneja huyo.
Pia
amesema kuwa kampuni ya SBC Tanzania imefanya punguzo hilo kuanzia
tarehe 16/11/2015 kwa vinywaji vya Pepsi, Mirinda,7up, Mountain Dew na
Evervess na maeneo yatakayo husika na punguzo hilo la bei ni Dar es
salaam,Morogoro, Dodoma, Pwani, Tanga, Lindi, Mtwara na Zanzibar.
“Ni
matumaini yetu mtaendelea kutuunga mkono katika biashara yetu kwa
kununua soda zetu kwa bei iliyopendekezwa ya shilingi Mia Tano kwa
chupa, shilingi elfu tisa mia nne (9,400) kwa kreti moja na faida kwa
wauzaji wa rejareja itakuwa ni shilingi 2500 kwa kila kreti” aliongeza
Bw. Chenja.
Mbali
na hayo Kampuni ya SBC Tanzania Limited inawashukuru wateja wake kwa
kuwaunga mkono katika biashara yao kwa kipindi cha miaka 14 hapa nchini.
Post a Comment