Dkt Hamisi Kigwangalla Mbunge Mteule Nzega Vijijini CCM. |
Mbunge mteule jimbo la Nzega vijijini Dkt Hamisi Kigwangalla (CCM) ametoa ushauri kwa wizara husika juu ya udhibiti
wa kuvuja kwa madawa serikalini na kwenda kwenye maduka binafsi.
Kupitia ukarasa wake facebook Kigwangalla amesema #SasaKaziTuChangamoto ya Udhibiti wa Kuvuja
Madawa Kutoka Mfumo wa Serikali Kwenda Kwenye Maduka ya Watu Binafsi ni Katika
Mambo ambayo mgombea Urais wa CCM, Ndg. John Pombe Magufuli alionesha kuwa
yanamkera sana. Hivyo wananchi wanasubiri kuona nini kitafanyika kutatua
changamoto hii...kuna 'expectation gap' ambayo ni lazima izibwe ndipo watu
wasadiki kushuhudia #MabadilikoYaKweli.
Nimesikia kuna mkakati wa kutaka kuondoa maduka yote jirani na hospitali za
serikali. Si wazo baya sana lakini ninaamini na ninajua kwa hakika kabisa kuwa
kuna suluhisho bora zaidi ya hilo.
Inawashangaza watu wengi kuwa kwenye pharmacy za watu binafsi nje tu ya
hospitali kuna dawa za kutosha za kila aina wakati kwenye pharmacy ya serikali
ndani ya hospitali hakuna! Kuna watalamu wetu wanadhani suluhisho ni kuzuia
uwepo wa pharmacy karibu zaidi na hospitali.
Ninafahamu kwa mfano, kuna tafiti
zimefanyika pale Muhimbili kuhusiana na idadi ya dawa zilizopo ukilinganisha na
pharmacy mojawapo pale nje; matokeo ya utafiti huo yakawa, Muhimbili kuna dawa
tofauti tofauti 850 (lines), wakati kwenye hiyo pharmacy kuna dawa tofauti
tofauti takriban 3200!
Unaweza kusema si busara kuziondoa pharmacy hizi wakati tunajua kabisa
kwenye hospitali yetu pale hakuna dawa za kutosha, maana itakuwa ni usumbufu kwa
wagonjwa wanaoagizwa kutafuta dawa fulani ambayo Muhimbili haipo.
Unaweza
kusema kuwa aina mbalimbali zaidi ya 2300 za madawa zimeibiwa kutoka Muhimbili,
na mimi hapo utanipa shida sana kukuelewa. Na nitakuuliza, zimepitia wapi
pamoja na ulinzi uliopo? Na kama ziliwahi kuweza kutoka nje ya hospitali mpaka
pharmacy, kwani pharmacy hiyo ikihamia Kariakoo ama Posta kutakuwa kuna ugumu
gani wa 'wezi' hao wa madawa kuzifikisha huko pia kama wameweza kuzitoa?
Nadhani njia hii ni too 'mechanical' na haitoondoa tatizo zaidi ya kuzalisha
tatizo lingine 'la usumbufu kwa wagonjwa'.
Nini kifanyike kudhibiti dawa zisikosekane kwenye mfumo wa afya?
1. Tuhakikishe tuna dawa za kutosha kwenye Idara ya Bohari ya Dawa (MSD) kwa
kuongeza 'capacity' yake kununua 'lines' nyingi zaidi za dawa kuliko ilivyo
sasa, ambapo MSD inaweza ku-supply only 65% ya mahitaji.
2. Bohari ijiendeshe kibiashara.
3. Tuweke 'color code' kwenye dawa zote za serikali kwenye bohari; mfano
labda dawa za serikali ziwe na rangi ya 'pink' pekee, na rangi hii iambatane na
'bar code', na kuwe na 'task force' maalum ya ukaguzi wa pharmacy za binafsi na
ikitokea dawa ya serikali ikakutwa kwenye pharmacy yoyote ile kuwe na adhabu
kali.
4. Bohari ya Dawa (MSD), kwa makubaliano maalum na hospitali husika, iruhusiwe
kufungua pharmacy zake kwenye hospitali zote nchini ili iuze moja kwa moja kwa
wateja. Tunaweza kuanza na hospitali chache za mfano - kama Muhimbili, Amana,
Mwananyamala, Temeke, Sekou Toure, Za Rufaa za Mikoa na baadhi ya Wilaya, Vituo
Vya Afya na Zahanati; Ili kuliko wateja wa hospitali za serikali kwenda kununua
dawa kwa bei ya kurusha kwenye pharmacy za watu binafsi kule nje wanunue kwa
bei nafuu ya serikali ndani ya hospitali zetu.
5. Tuongeze kasi ya kusajili wananchi wote kwenye Mfumo wa Bima ya Afya kwa
Wote ili kuongeza financing kwenye mfumo wa afya wa serikali zaidi ya kutegemea
bajeti tu.
6. MSD wakiishakuwa na pharmacy yao ndani ya
health facility watakaa na wataalamu na menejimenti ya hospitali husika na
kuorodhesha madawa wanayohitaji na MSD kuhakikisha yapo kwenye pharmacy yao
kwenye kituo husika.
(JAMIIMOJABLOG)
Post a Comment