Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue atafanya ziara katika Hospitali ya
Taifa Mhimbili Kesho Jumatatu (23 Novemba, 2015) kuanzia majira ya saa
nne asubuhi.
Ziara
hiyo ni kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
aliyeagiza fedha zilizochangwa ajili ya hafla ya wabunge zitumike
kununulia vitanda vya wagonjwa katika hospitali hiyo.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasilino, IKULU
20 Novemba, 2015
Post a Comment