Miss Tanzania aliyeshika nafasi ya pili, 2014 Jihan Dimack akiwa kwenye ‘red carpet’ iliyokuwa imeandaliwa.
… Jihan akihojiwa kwenye ‘red carpet’ iliyokuwa imeandaliwa .
Mrembo huyo akipiga picha za pozi na mashabiki kwenye ‘red carpet’.(P.T)
Mashabiki wakipiga picha za pozi kwenye ‘red carpet’ .
Mwanamitindo, Miriam Odemba akipiga picha za pozi kwenye ‘red carpet’.
Miriam (kushoto) akifanya mahojiano.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ben Pol (kushoto) akipiga picha za pozi na watu mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo
Meza kuu ya Majaji wa shindano hilo.
Warembo wakipita mbele ya majaji kuonesha ujuzi wao.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi (mbele) akizungumza jambo.
Washiriki wakibakia wanne kumpata mshindi.
Maria Sarungi akimvalisha taji la Ushindi Mshindi wa Miss Universe 2015, Lorraine Marriot .
Kutoka kushoto ni mshindi wa tatu, Willice Donald kutoka (Dar), mshindi wa pili, Lilian Loth (Dar) na mshindi wa kwanza, Lorraine Marriot.
Wakiwa wametokelezea na mataji yao.
Majaji wa shindano hilo wakiwa katika picha ya pamoja na warembo hao.
….wakiwa kwenye picha ya pamoja.
SHINDANO la Miss Universe Tanzania 2015 jana Ijumaa, lilifikia tamati baada ya mmoja ya waliokuwa washiriki wa shindano hilo, Lorraine Marriot kuibuka kidedea akiwabwaga wenzake 14 waliokuwa wakichuana.
Mashindano hayo yalimalizika jana usiku kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga , jijini Dar ambapo ilikuwa fainali na muandaaji akiwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi .
Aidha katika mashindano hayo warembo hao walitoka mikoa mbalimbali walishiriki kuwania taji hilo ambao miongoni mwao ni Mariam Isack, Lilian Loth, Stacey Sulul , Willice Donald, Marriot, Darena David , Mercy Zephania, Dinnah Kaijage, Melody Typhone wote hawa wakitokea mkoa wa Dar es Salaam.
Wengine walioshiriki ni Joselyn Mirashi (Arusha) , Nancy Matta (Mbeya), Christina Shimba (Iringa) na Beinda kutoka Mwanza.
NA DENIS MTIMA/GPL
Post a Comment