Wizara ya ugatuzi imekabiliwa na tuhuma nyingi za ufisadi karibuni
Waziri
mwenye ushawishi mkubwa katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta
amejiuzulu wadhifa wake baada ya shinikizo kutolewa ajiuzulu kutokana
natuhuma za ufisadi.
Bi Anne
Waiguru, ambaye amekuwa Waziri wa Mipango na Ugatuzi, ameambia
wanahabari Nairobi kwamba ameshauriwa na daktari wake “achukue muda
kupumzika”.
Amewaambia wanahabari kwamba amemwandikia Rais Kenyatta akimtaka amuondolee majukumu yake.
Wakenya wapigania waziri kwenye Twitter
Hata hivyo amesisitiza kwamba hana hatia.
“Ninafuata
ushauri wa daktari na nimemuomba Rais aniondolee majukumu yangu kama
waziri ... na akiona inafaa, anipe majukumu ambayo si mazito,” Bi
Waiguru amesema.BBC
Post a Comment