Waziri
mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa, amesema
hakuwa na taarifa yeyote juu ya uteuzi wake uliofanywa na Rais.
Akizungumza
na Azam TV, Mheshimiwa majaliwa amedai usiri uliotumika ni mkubwa ambao
hata yeye atauendeleza katika kuimarisha Serikali.
“Huwezi amini mpaka asubuhi nafanya zoezi na Wabunge wenzangu sikuwa najua lolote, mimi ni kocha wa timu ya mpira ya Bunge.
"Yani
mpaka Spika ameanza na ile Ruangwa nikapigwa na butwaa, na nimelia kwa
sababu sikuamini kilichotokea, ila ndo hivyo Rais ameniamini akanipa
nafasi” alisema Mh. Majaliwa.
Post a Comment