Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban
Mwinjaka,akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Rwanda, Rwakunda
Christian,wakati walipotembelea ujenzi wa reli mpya ya kisasa, iliyoanza
kujengwa Mkoani Pwani, katika eneo la Soga.
Muonekano wa ujenzi wa reli mpya wa kisasa Standard Gauge, ambayo inaendelea
kujengwa katika eneo la soga mkoani Pwani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban
Mwinjaka (wa tatu kutoka kulia), akiwa katika picha pamoja na Uongozi wa
Taasisi inayosimamia usafirishaji katika Ukanda wa Kati pamoja na Viongozi wa
Nchi zinazotumia ukanda wa Kati, wakati walipotembelea ujenzi huo hivi
karibuni, katika eneo la Soga, Pwani.
Muonekano wa Vituo vya Reli hiyo Mpya ya kisasa ya
standard Gauge, itakapokamilika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Rwanda,
Rwakunda Christian, akiteta jambo na maafisa kutoka nchi zinazotumia ukanda wa
kati kusafirisha bidhaa zao, wakati wakiangalia ramani ya reli mpya ya kisasa,
walipotembelea ujenzi wa reli mpya ya kisasa ya standard gauge, hivi karibuni Mkoani Pwani. Viongozi hao
walifurahishwa na maendeleo ya ujenzi huo kwa sababu utarahisisha usafirishaji
wa mizigo kwani itapitisha mzigo zaidi na ukubwa wa reli hiyo utaongeza spidi
ya treni.(Habari Picha na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini-Uchukuzi)
Post a Comment