Mwanajeshi feki wa jeshi la wananchi(JWTZ)amekamatwa leo Mkoani Kigoma akiwa amevaa sare za jeshi hilo.
Akiongea
na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya tukio hilo kamanda wa
polisi wa Mkoa wa Kigoma Fednandi Mtui alisema kuwa mwanajeshi huyo feki
alikamatwa jana eneo la kazuramimba katika Wilaya ya uvinza.
Mtui
alisema kuwa mwanajeshi huyo alitambulika kwa jina la James Charles
miaka 27 mkazi wa kijiji cha Nyamori alikamatwa baada ya kuwepo kwa
taarifa kutoka kwa raia wema juu ya utapeli aliokuwa akiwafanyia na
kuwekewa mtego na kukamatwa.
Kamanda
alisema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kuhojiwa na kuulizwa alipozitoa
sare hizo alisema kuwa yeye ni dobi wa kufua nguo,hivyo huvaa sare hizo
pale anapoletewa na wateja kwaajili ya kuzifua.
Alisema
mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika,pia jeshi la
polisi limetia wito kwa wananchi wote ambao wameshatapeliwa na
mtuhumiwa huyo kutoa taarifa katika kituo chochote cha polisi kilichopo
jirani yao.
Post a Comment