Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KAULI YA UONGOZI WA DIAMOND PLATNUMZ KUHUSU MANENO YA ALIKIBA INSTAGRAM

Baada ya Alikiba kupost ujumbe katika Instagram akidai kuwepo na mambo yanayoendelea nyuma ya pazia kwenye muziki wake na wengi kutafsiri amelalamikia kukosa tuzo za Afrima, uongozi wa Diamond aliyeshinda tuzo tatu umezungumza.
Akizungumza katika pindi cha XXL cha Clouds FM, mmoja kati ya mameneja wa Diamond, Babu Tale alisema walisikitishwa na ujumbe huo.“Mimi naona asiyekubali kushindwa sio mshindani,” alisema. “Hata sisi tumeshawahi kuingia kwenye tuzo ambazo na yeye aliongea maneno hayo alikuwepo na akashinda na hakuna mtu yeyote aliongea sijui mmenunua tuzo. Mimi nilijua mashabiki ndio wanaongea mpaka msanii anapost kitu kama kile nikahisi labda kuna mtu amehack akaunti yake. Kwahiyo nilivyoona vile nikamhukumu sio mshindani,” alisema Tale.
Hata hivyo Tale alisema baada ya kufuta kauli hiyo na kuzungumzia kauli hiyo aligundua huenda alishinikizwa na mashabiki wake.
“Lakini baadaye baada ya kuona ameongea vizuri, nikagundua sometimes mtu anaweza kupaniki kwa ajili ya mashabiki wanaoongea. Lakini mwisho wa siku tunatakiwa tukae meza moja ili tusukume muziki wetu wa Tanzania. Tukiangalia line up ya muziki wa Afrika sasa hivi tupo namba mbili, tunakwenda kwenye namba 1,” aliongeza.
Hata huvyo Alikiba aliifuta post hiyo na kudai kuwa hakuandika kwa sababu alikosa tuzo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top