JUMLA ya watu 87 katika wilaya ya Bahi katika Mkoa wa Dodoma wamegundulika kuwa na ugonjwa wa kipindupindu.
Dk.
Maro amesema mgonjwa wa kwanza aligundulika Oktoba 21 mwaka huu ambaye
alitokea kata ya Mpamatwa ambapo wagonjwa wengine waliendelea kujitokea
hadi kufikia 81 hadi sasa.
Hata
hivyo amesema wagonjwa wengine sita wa kipindupindu walitokea kata ya
Bahi Makulu na kata ya Mtitaa na kufanya wagonjwa wote kufikia 87 hadi
leo.
Akitoa
ufafanuzi amesema hadi jana wagonjwa watatu ndiyo pekee wamelazwa
katika kambi maalum ya kuwashughulikia wagonjwa hao huku wagonjwa wa
kipindupindu 84 wakiwa wameruhusiwa na kurudi majumbani kwao.
Akizungumzia suala ya kujitokeza kwa maambukizi hayo amesema ni kutokana na kuwepo kwa tatizo la maji yasiyo safi na salama.
“Hapa
Bahi kuna tatizo kubwa la uhaba wa maji safi na salama kutokana na hali
hiyo watu wanatumia maji ya kisima vifupi ambavyo kimsingi maji yake si
salama sana.
“Hata
hivyo kutokana na hali ya kuzuka kwa kipindupindu uongozi umefanya kila
jitihada za kuhakikisha maji yanatibiwa na kwa sasa visima vyote vya
maji vimewekewa dawa ya kutibu maji,” amesema Dk. Maro.
Jambo
lingine lililochangia mlipo wa ugonjwa huo, amesema ni tatizo kubwa la
kaya nyingi kutokuwa na vyoo bora jambo ambalo linaweza kusababisha
kuwepo kwa mlipuko wa magonjwa kama hayo.
Dk.
Maro amesema kwa sasa wananchi wanapatiwa elimu ya kuhakikisha wanaishi
katika mazingira salama ikiwa ni pamoja na kuwa na vyoo ambavyo ni bora
kwa lengo la kujiepusha na mlipuko wa magonjwa kama hayo.
Mbali
na hilo amesema viongozi wa kata mbalimbali ambao wanatoka wagonjwa
wanaimizwa kutoa elimu kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuimiza swala la
usafi ili kuifanya jamii kuwa katika mazingira ambayo ni salama zaidi.
Katika mkoa wa Dodoma kwa sasa watu wawili kutoka kata ya Mkoka wilayani Kongwa wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
Post a Comment