SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza kiingilio cha shilingi Elfu
moja (1,000) ndio kitakachotumika kuingia kushuhudia mchezo wa kirafiki
wa Kimataifa kati ya Timu ya Taifa Wanawake ‘Twiga Stars’ dhidi ya timu
ya Taifa ya Wanawake Malawi utakaochezwa kesho Jumamosi, Novemba 7
katika uwanja wa Azam Chamazi.
Twiga
Stars inayonelewa na kocha mzawa Rogasian Kaijage iliingia kambini wiki
iliyopita ambapo imekua ikifaya mazoezi kila siku katika uwanja wa
Karume kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa.
Katika
mchezo huo, Twiga Stars itautumia nafasi hiyo kumuaga mshambuliaji wake
wa siku nyingi Estha Chaburuma ambaye ni miongoni mwa waanzilishi wa
Twiga Stars na sasa anastaafu rasmi kucheza mpira wa miguu.
Upande
wa timu ya Taifa ya Malawi tayari imewasili jana jioni jijini Dar e
salaam ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 pamoja na viongozi nane ambapo
leo jioni kikosi chake kitafanya mazoezi katika uwanja wa Karume saa 10
jioni.
Post a Comment