Kwa
mara ya kwanza toka nimekatwa mguu miaka 6 iliyopita leo nimechukua
nafasi hii kupost hii pic kuondoa maswali mengi yaliyopo vichwani mwa
watu
Nipo kama unavyoiona pic
Huyo ndio wastara nilivyo hakuna kilichopungua zaidi ya hicho unachokiona
Kuwa mlemavu ni kitu kingine tofauti ukiwa mzima hivyo kusikia maumivu na kuumwa mguu ni kitu cha kawaida
Sasa
nipo nairobi kimatibabu na tatizo ni operetion ya kwanza nilikosewa
ndio sababu ya maumivu ya mara kwa mara madaktari wameshajua nini cha
kunifanya ili kuondoa mateso kwangu
Jifunze
kitu kupitia hii pic yangu na si kucoment ujinga jiulize ungekuwa wew
mama yako dada yako mume,mke, wako ungeweza kusmile kma mimi hali ya
kuwa una maumivu?
Jifunze kitu kupitia wastara
na sijajidharirisha nimetaka wewe unijue nilivyo ili usiteseke na maswali juu yangu
Sijakatwa
miguu yote kma ilivyovumishwa na pia pamoja na maumivu ninaweza
kutembea japo si mwendo mrefu sana na naendelea kusmile
SOTE TUSEME ALHMADULILAH
ASANTE MUNGU
Kwa Undani
2 hours ago
Post a Comment