Mabasi ya mwendokasi kuanza kazi rasmi mwezi Desemba kwenye barabara ya Kilomita 20.9 ya Kimara mpaka Kivukoni.
Mkurugenzi mkuu wa wa UDA-RT, kampuni inayohusika na usimamizi wa mabasi
hayo amesema wanamalizia baadhi ya mambo ili mradi huo uanze kufanya
kazi rasmi.
Amesema mabasi hayo tayari yameshawasili hapa nchini, kitu kilichobakia
ni kuweka mfumo wa kieletroniki utakaokuwa unajiendesha wenyewe wa
kulipa nauli kwa abiria.
Amesema pia tani kumi ya mageti yatakayowekwa kwenye sehemu abiria
watakapopandia mabasi hayo, yamewasili nchini jumatano ijayo, yataanza
kufungwa siku yoyote na ujenzi huo utamalizika ndani ya wiki tatu.
Mpaka sasa UDA-RT imepokea mabasi 140, mabasi 101 kati ya hayo yana
uwezo wa kubeba abiria 150, yaliyobaki yana uwezo wa kubeba abiria 80
tu.
Mradi huo utasaidia na kurahisisha adha ya usafiri Jijini Dar
Post a Comment