Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa amepiga marufuku mikutano yote ya
kisiasa na maandamano ya kisiasa kipindi ambacho Bunge la 11 litaanza.
Amesema
kuwa amri hiyo pia imetolewa na vyombo vya ulinzi na usalama ili
kuthibiti wale wote wenye malengo ya kuharibu amani na utulivu uliopo.
Wabunge
wateule wameanza kuwasili Dodoma kwa ajili ya kuapishwa na kusubiria
hotuba ya Rais Magufuli pamoja na Uchaguzi wa Spika na Naibu wake.
Galawa amesema yeyote atakaye jaribu kuharibu amani na utulivu uliopo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Post a Comment