Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LEO ALHAMISI NI SIKUKUU NA SIKU YA MAPUMZIKO


     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko. 

     Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muung ano wa Tanzania. 

     Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatano, Novemba 4, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana Sefue, Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa.

 Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.


4 Novemba, 2015
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top